Wednesday, May 28, 2014

Picha inayodaiwa kuleta kizaazaa.
Bondia Floyd Mayweather akifunguka katika mahojiano na necolebitchie.com.
BONDIA Floyd Mayweather amefunguka kuwa hajawahi kulala na mpenzi wa rappa T.I aitwaye Tiny.
Mayweather ameyasema hayo ikiwa ni siku chache tangu ugomvi kati ya kundi lake na T.I utokee kisa kikitajwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi kati ya bondia huyo na Tiny.
Katika mahojiano na mtandao wa necolebitchie.com, Floyd amesema hajawahi kulala na Tiny.
“Sijawahi kumbusu wala kumgusa Tiny katika mazingira yenye utata. Rafiki yake aitwaye Shekinah alihitaji kuja kwenye pambano na akaja na Tiny. Hivyo walikuja kushuhudia mpambano,” alisema Floyd.
Tiny alitupia picha yake, Shekinah, Floyd na wengine kwenye mtandao wa Instagram ambayo Floyd anaamini ndiyo iliyoleta kizaazaa.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe