
Supastaa Neymar.
VITA kubwa imeibuka kati ya klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil kuhusu supastaa Neymar.
Miamba ya soka Hispania, Barcelona wanataka
kumtumia Mbrazili huyo kwenye mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Atletico
Madrid kwenye Ligi Kuu Hispania wakiamini watashinda ili kunyakua
ubingwa, wakati Brazil hawataki acheze kwa hofu ya anaweza kuumia kabla
ya kuanza fainali za Kombe la Dunia kwa sababu ndiye tumaini lao kubwa.
Barca wanataka Neymar acheze kwa sababu ndiye
mchezaji pekee aliyefunga bao walipomenyana na Atletico msimu huu na
hivyo wanamini ataendeleza makali yake dhidi ya kikosi hicho
kinachonolewa na Muargentina Diego Simeone.
Chama cha soka Brazil na wadhamini wa supastaa
huyo hawataki acheze kwa sababu jambo hilo linaweza kumsababishia
majeruhi yatakayomfanya akose fainali za Kombe la Dunia.
Nchini Brazil, Neymar si mchezaji wa kawaida tu,
bali ni kipenzi kikubwa wa vyombo vya habari vya nchi hiyo na kwamba
makampuni mengi yamekuwa yakicheza kamari kuhakikisha staa huyo
anakuwapo kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia zitakazoanza mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment