
KIFO cha nyota wa filamu Bongo, Adam Kuambiana kilitibua sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya watoto wawili Nicole na Martin iliyoandaliwa na Aunt Ezekiel akiwa na shoga yake Wema Sepetu.
Mastaa hao walikuwa wamekamilisha kila kitu na walishaanza shamrashamra zaa, ghafla wakasikia taarifa za kifo cha Kuambiana.
“Mi naumia jamani, unajua filamu yetu ya mwisho tuliyocheza mimi na Wema, yeye alikuwa dairekta. Yaani tulikuwa tukimchezea kama babu yetu, hebu angalia hii clip,” alisema Aunt huku akimwonyesha mwandishi wetu clip hiyo kwenye simu yake.
Hata hivyo kwa kuwa walikuwa wameshatayarisha kila kitu huku waalikwa wakiwa eneo la tukio, walimalizia hafla hiyo ingawa machozi yakitawala badala ya furaha.
0 comments:
Post a Comment