Ivo upo? Msikie huyu Mzee Mtemi hapa
MWAMUZI mkongwe nchini Idd Ngongite ‘Mtemi’ ametamka wazi kuwa
kama yeye angekuwa anachezesha sasa mechi za Ligi Kuu basi kila mechi
angekuwa akimpa kadi za njano kipa wa Simba Ivo Mapunda kutokana na
kuingia na taulo lake uwanjani.
Ngongite ambaye alitamba katika miaka ya 70
alisema angeweza kumhukumu kwa sheria namba 4 sheria kati ya zile 17
ambazo zinaonyesha mavazi na vitu ambavyo mchezaji anatakiwa kuingia
navyo uwanjani lakini kati ya hivyo taulo halipo.
Akizungumza na Mwanaspoti mjini hapa Ngongite
alisema sheria namba 4 ya mavazi kwa mchezaji inajieleza vitu ambavyo
anatakiwa kuwa navyo ambavyo ni jezi,glovu na vifaa vingine kama vizuia
ugoko lakini, haielezi kuingia na vitu vingine kama taulo.
“Nimeona hata Ulaya waamuzi wanashindwa kuwapa
adhabu hawa wachezaji wanaoingia na mataulo uwanjani kwa kuwa kwanza
havijakaguliwa na pili sheria namba 4 ya mavazi haijaruhusu. Sasa kama
mimi angekuwa anakutana na kadi za njano kila mechi ule ni ubishoo tu
taulo anayetakiwa kuna nalo ni daktari wa timu tu,”alisema Ngongite.
0 comments:
Post a Comment