Cristiano
Ronaldo (kushoto) akishangilia bao lake la penalti dhidi ya Atletico
Madrid. Kulia ni Mario Balotelli alipofunga bao katika nusu fainali ya
Euro 2012 kati ya Italia na Ujerumani.
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ‘amekopi na kupesti’
staili ya mshambuliaji wa AC Milan Mario Balotelli baada ya kufunga bao
la nne dhidi ya Atletico Madrid kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
usiku wa kuamkia leo.
Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao la nne dhidi ya Atletico Madrid.
Ronaldo baada ya kufunga bao hilo kwa penalti, alishangilia kwa kuvua
jezi na kisha kutunisha misuli kama alivyofanya Balotelli alipofunga
bao katika nusu fainali ya Euro 2012 kati ya timu yake ya Taifa Italia
na Ujerumani.
Baada ya tukio hilo, Ronaldo alionyeshwa kadi ya njano japo
hakuonekana kujali. Kwenye fainali hiyo, Real Madrid walishinda kwa bao
4-1 na kutwaa kombe.
0 comments:
Post a Comment