Thursday, May 8, 2014

BASATA YAWAPIGA STOP BONGO MOVIE

Stori: Adamu Mwanakatwe!

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapiga stop waigizaji wa filamu nchini kuacha mara moja tabia ya kuendesha miradi ya uibuaji wa vipaji (Talent Search) bila kwanza kupata kibali kutoka kwa taasisi hiyo ya serikali.

Steve Nyerere.
Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya wasanii kadhaa wa filamu kwenda mkoani Mwanza na kuendesha ‘project’ hiyo zenye lengo la kuibua mastaa wapya kwa ajili ya ushiriki kwenye kazi zao. Kabla ya ziara ya hivi karibuni, hapo nyuma pia wasanii kadhaa wamewahi kuripotiwa kuendesha miradi hiyo katika mikoa mbalimbali.
Akizungumzia suala hilo, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Lebejo Mngereza alisema ni kinyume cha sheria kwa mtu au kikundi chochote, kuendesha tukio lolote la kisanaa bila kupata kibali cha taasisi hiyo, kwani ndiyo yenye jukumu la kusimamia masuala yote ya sanaa na utamaduni nchini.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe