Friday, April 18, 2014

PROFESSOR LIPUMBA ALIVYOLIAGA BUNGE..NOMA SANA!

 

Badhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba walio katika Umoja wa UKAWA   jioni ya leo wameamua kutoka nje wakati wajumbe wakiendelea na majadiliano ya taarifa za kamati ya bunge hilo   kuhusu sura ya kwanza na ya sita. 



Hatua hiyo imefikiwa na wajumbe hao baada ya kuunga mkono mchango wa Profesa Lipumba ambaye amesikitishwa na jinsi   mjadala wa bunge hilo unavyogubikwa na ubaguzi.
Profesa Lipumba amesema wanahitaji katiba itakayo hakikisha   kila mwananchi anapata haki yake bila kujali rangi jinsia na makabila msingi alioucha baba wa Taifa hayati  Mwalimu Julius Nyerere.
Aidha Profesa Lipumba alieza kuwa amesikitishwa na Kauli iliyotolewa na   Waziri William Lukuvi wakati wa sherehe ya  kumsimika mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu akimwakilisha Waziri Mkuu.


0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe