LIGI KUU BARA 2013/14: Ilikuwa kaazi kweli kweli...!
>Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe laubingwa wa Ligi Kuu Bara na Rais wa TFF, Jamal Malinzi juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Mbagala Dar es Salaam na kuandika historia ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza.
MBIO za Ligi Kuu Bara msimu wa 2013/14 zimefikia tamati Jumamosi
iliyopita na kuishuhudia Azam FC ikiibuka bingwa na kuweka historia ya
kuzipiku timu kongwe za Simba na Yanga zilizokuwa zikipokezana taji hilo
miaka nenda rudi.
Azam pia imeweza kuizima timu ya Mbeya City ambayo imeshiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza.
Yawezekana ndiyo ligi iliyokuwa na ushindani wa
hali ya juu kati ya zote zilizochezwa ndani ya miaka mitano au 10 ya
karibuni kutokana na ushindani ulioonyeshwa na klabu shiriki huku mabao
402 yakifungwa.
Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe raia wa Burundi ndiye aliyeibuka kinara wa ufungaji baada ya kupachika wavuni mabao 19.
Timu 14 zilishiriki ligi hiyo, Azam imekuwa bingwa
na kukata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, Yanga
imeshika nafasi ya pili na mwakani itacheza Kombe la Shirikisho huku
kilio kikibaki kwa timu tatu za Rhino Rangers, JKT Oljoro na Ashanti
United zilizoshuka daraja.
Ufuatao ni ushiriki wa timu 14 katika ligi hiyo;
Azam
Azam imeweka rekodi kwa kutwaa ubingwa bila
kufungwa, imefikisha pointi 62 katika mechi 26 na kuandika rekodi mpya.
Timu hiyo iliyomaliza kwenye nafasi ya pili mfululizo misimu miwili
iliyopita, ilianza ligi kwa kusuasua kidogo baada ya kukwamishwa na sare
katika mechi za mwanzo kabla ya kucharuka baadaye na kupanda kileleni.
Timu hiyo, mali ya kundi la makampuni ya S.S
Bakhresa, ilicheza soka safi mzunguko wa kwanza chini ya Kocha Stewart
Hall na kumaliza mzunguko huo wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Yanga
iliyokua kileleni. Baadaye ikaachana na Hall na kumuajiri Joseph Omog
aliyefanikiwa kuiongoza katika mechi 13 zilizobaki bila kupoteza na
kunyakua ubingwa.
Yanga
Klabu kongwe, ilijitahidi kuhakikisha inatetea
ubingwa wake lakini haikufanikiwa, ilimaliza ikiwa ya pili na pointi 56
huku ikiweka rekodi ya kufunga mabao 61 Azam ikifunga mabao 51. Sasa
haitacheza Ligi ya Mabingwa Afrika badala yake itacheza Kombe la
Shirikisho. Mzunguko wa kwanza ilikuwa chini ya Ernest Brandts na
ilimaliza hatua hiyo ikiwa inaongoza ligi kabla ya kumtimua Brandts na
mzunguko wa pili walimpa kazi Hans Van Der Pluijm. Yanga ilikuwa hatari
kwa timu za jeshi baada ya kuzifunga mabao 7-0 (Ruvu Shooting), ikaipiga
Prisons 5-1 kisha ikaifunga JKT Ruvu 5-1. Iliwania ubingwa hadi dakika
ya mwisho lakini kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Mgambo JKT kiliharibu
mambo.
Mbeya City
0 comments:
Post a Comment