Jaji Samatta, Prof Lumumba kutumika kuwarejesha Ukawa bungeni
Huwezi kuwalazimisha watu kuamua jambo ambalo hawalitaki kama ni muundo wa Muungano tunaomba wananchi ndiyo waamue, lakini yote hayo Katiba yetu inatakiwa kubainisha mambo mbalimbali yanayohusu watu wenye ulemavu na haki zao zote,”
Wiki hii Bunge Maalumu la Katiba limeahirishwa, kupisha Bunge la
Bajeti kuanza vikao vyake vya bajeti kwa mwaka mpya wa fedha wa
2014/15.
Hata hivyo, Bunge hilo limeahirishwa likiwa
limegawanyika vipande, baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kutoka nje ya Bunge hilo Aprili 16, wakipinga kejeli,
matusi na mambo mengine ya ukiukwaji wa taratibu yaliyokuwa yakifanywa
na baadhi ya mawaziri nje ya Bunge.
Kutoka kwa Ukawa nje unaojumuisha vyama vya
Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, DP na wajumbe 25 kutoka kundi la 201
hakukuzuia Bunge hilo kuendelea na vikao vyake. Bunge hilo limeahirishwa
Agosti 5, litakapokutana tena mjini Dodoma kuendelea na majadala wa
kuijadili Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba.
Kundi la Tanzania Kwanza linalojumuisha wajumbe
wengi wa CCM, wamekuwa wakiwapiga vijembe kuwa warudi bungeni kuendelea
na mjadala huo kwani Katiba haitengenezwi nje ya Bunge.
Jukata yasaka suluhu
Kutokana na mgawanyiko huo kuonyesha kuligawa
taifa na kuwaacha wananchi wakiwa njiapanda juu ya hatima ya kupata
Katiba Mpya, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) linajipambanua kutaka
kusaka suluhu ya mvutano huo.
Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba anasema, Jukwaa
hilo linajitolea kusaka suluhu kwa kuratibu maridhiano ya makundi
yanayovutana ya Ukawa na la Tanzania Kwanza.
Anasema lengo la kusaka maridhiano hayo ni
kuhakikisha kabla ya Bunge hilo kuanza Agosti 5, kunakuwapo maridhiano,
yatakayowezesha wajumbe wote wanakuwa kitu kimoja katika kujadili
maudhui ya rasimu, licha ya tofauti zao za kiitikadi na kimisimamo.
Kibamba anasema wameamua kuwaalika wataalamu ambao
wana uzoefu wa siku nyingi katika masuala ya sheria kusimamia
maridhiano hayo, yatakayojenga umoja na mshikamano katika taifa.
Wataalamu hao kwa mujibu wa Kibamba ni Jaji Mkuu
Mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta anayekuwa mwenyekiti, Profesa
Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msuluhishi mwenza
sambamba na uwepo wa makundi ya viongozi kutoka Ukawa, Tanzania Kwanza,
vyama vya siasa, asasi za wananchi na taasisi zote muhimu zilizoguswa na
mchakato huu.
“Katika kujenga Katiba yenye kuwajali wananchi,
tunaomba kila upande kuridhia kukutana na kutokuwa na misimamo mikali
ili kuhakikisha tunawaunganisha na kuendelea na mchakato huo kama
kawaida,” anasema Kimbamba.
Kuhusu uhalali wa Bunge hilo kuendelea na mijadala
licha ya Ukawa kutoka nje, anasema sheria za Jumuiya ya Madola kwa
mabunge ya Katiba kundi moja linapotoka nje kwa tamko, Bunge hilo
hutakiwa kusitishwa
0 comments:
Post a Comment