Ronaldo ashitua kumwita Irina mkewe

Ronaldo akiwa na mpenzi wake, kwenye tuzo za mwanasoka bora wa dunia
SUPASTAA, Cristiano Ronaldo ameibua mapya kwenye sherehe za
utoaji wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka zilizofanyika Uswisi
Jumatatu iliyopita baada ya kumtambulisha mpenzi wake, mrembo Irina
Shayk kuwa ni mkewe.
Utata ulioibuka kama staa huyo wa Real Madrid kama
atakuwa amemuoa kwa siri mrembo huyo wa Kirusi anayejihusisha na
masuala ya mitindo.
Ronaldo baada ya kutajwa mshindi na kuwabwaga
wapinzani wake, Lionel Messi na Franck Ribery kwenye hotuba yake ya
kushukuru, alimtaja Irina kuwa mkewe jambo lililowashitusha wengi
ukumbini hapo.
Mreno huyo aliaambatana na Irina kwenye tuzo hizo
pamoja na mtoto wake na alipotajwa tu kuwa ameshinda, alimbusu mpenzi
wake kwanza kabla ya kwenda jukwaani na mwanaye, Cristiano Jr
kuwashukuru wachezaji wenzake, familia na “mkewe”.
Ronaldo alisema: “Namshukuru kila mtu aliyehusika
na mimi kwenye viwango tofauti. Mke wangu, marafiki zangu na mwanangu.
Hili ni tukio lenye hisia kubwa.”
Ronaldo amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo huyo wa Urusi tangu 2010.
0 comments:
Post a Comment